Saturday, July 17, 2010

Amuosha Mwanae Kwenye Mashine ya Kufulia Nguo.


Mwanamke mmoja nchini Japan amewashtua watu wengi nchini humo baada ya kukiri kuwa alikuwa akimuosha mtoto wake wa kike wa miaka mitano kwenye mashine ya kufulia nguo ili kumfundisha adabu.


Junko Egashira mwenye umri wa miaka 34 aliwaambia polisi wa magharibi mwa Fukuoka nchini Japan kuwa mara kadhaa alikuwa akimweka mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka mitano kwenye mashine ya kufulia nguo na kisha aliiwasha mashine hiyo.

Mwanamke huyo alisema kuwa alikuwa akifanya hivyo ili kumtia adabu mtoto huyo anapoleta utundu.

Junko aliwaambia polisi kuwa alikuwa akiifunga pamoja mikono na miguu ya mtoto wake na kuuziba mdomo wake kwa kutumia gundi ya platiki na kisha kumweka ndani ya mashine ya kufulia nguo na kuiwasha mashine hiyo kwa dakika kadhaa.

Katika mojawapo ya mateso ambayo Junko alikuwa akimfanyia binti yake ni kuifunga mikono yake kwa kamba na kisha kumweka mtoto huyo ndani ya ndoo iliyojaa maji.

Mtoto huyo alifariki dunia juni 27 baada ya mama yake kumfunga kamba shingoni na kisha kumning'iniza ukutani.

"Nilimfunga kamba shingoni na nilimning'iniza ukutani baadae nilimkuta amefariki, sikufikiria kama angefariki", Junka aliwaambia polisi.

Junka alianza kuishi na binti yake huyo miaka miwili iliyopita baada ya kutengana na mumewe.

Junka anakabiliwa na mashtaka ya mauaji.




HARUSI YA AIBU...

Na Waandishi Wetu
Miongoni mwa matukio ya aibu yaliyowahi kujiri kwa mwaka 2010, ni hili la ndoa kati ya kijana aliyefahamika kwa jina la Suleiman Salum Mazinge na Pili Saidi, wakazi wa Mwananyamala, Dar es Salaam iliyotarajiwa kufungwa Julai 9, mwaka huu iliyoeyeyuka dakika za mwisho, Amani lina ‘A-Z’ ya tukio zima.

Taarifa za awali zilizotufikia kutoka kwa chanzo chetu makini zilidai kwamba, ndoa hiyo iliyokuwa imetawaliwa na maandalizi ‘babkubwa’ ilitarajiwa kufungwa katika Msikiti wa Mwananyamala ‘B’, lakini cha ajabu muda mfupi kabla ya mashehe kutia ubani, mambo yaliharibika baada ya zoezi la wawili hao kupima afya zao kushindikana.


Ilielezwa kuwa, Pili na Suleimani wamekuwa wapenzi kwa muda mrefu na kufuatia penzi lao kunoga, waliamua kuchukua hatua za kuoana ambapo taratibu za kufanya hivyo zilianza mara moja.

“Mazinge akatuma mshenga aliyefahamika kwa jina la Mzee Mfundo ambaye ni babu yake lakini pia mjumbe wa nyumba kumi na baada ya siku chache upande wa msichana uliridhia binti yao kuolewa,” kilisema chanzo hicho.

MTOTO ATEKETEA KWA MOTO MANZESE.

Mwili ukiondolewa eneo la tukio.
MTOTO Abdulrazak Noel (4) wa Manzese jijini Dar es Salaam, jana usiku aliteketea kwa moto baada ya mama yake kumfungia chumbani na kwenda kufanya biashara ya Mama Lishe. Mashuhuda walidai chanzo cha moto huo ni kulipuka kwa kibatari.


Mmoja wa mashuhuda akiangalia mwili wa marehemu.


Umati ukishuhudia tukio hilo.


Wananchi wakishirikiana na polisi kuuingiza mwili kwenye ‘Difenda’ kwa ajili ya kuhifadhiwa.

Mambo ya kawaida jamani...

Kama unaona kuwa kuna kitu kinakufurahisha humu kwenye blog yangu basi hakuna noma kama ukiniangushia sifa mwanangu mwenyewe.....
Washkaji Mungu akipenda tutaonana basi.........ila kumbuka kuwa Mungu ni mmoja na siku zote anafanya maajabu kwahiyo si mbaya kama tukimshuru kwa kila nia.....
Mungu awabariki watu wote wa Dunia hii.Amen!

9 Things I Hate About Everyone

1. People who point at their wrist while asking for the time.... I know where my watch is pal, where the hell is yours? Do I point at my crotch when I ask where the toilet is?



2
 People who are willing to get off their ass to search the entire room for the T.V.. remote because they refuse to walk to the T.V. and change the channel manually. 

3
 When people say 'Oh you just want to have your cake and eat it too'. Damn right! What good is cake if you can't eat it? 

4
 When people say 'it's always the last place you look'. Of course it is. Why the hell would you keep looking after you've found it? Do people do this? Who and where are they?   cause I amGonna Kick their asses! 

5
 When people say while watching a film 'did you see that?'. No Loser, I paid $12 to come to the cinema and stare at the damn floor. 

6
 People who ask 'Can I ask you a question?'.... Didn't really give me a choice there, did ya sunshine? 


7.
 When something is 'new and improved!'. Which is it? If it's new, then there has never been anything before it. If it's an improvement, then there must have been something before it, couldn't be new.

8
 When people say 'life is short'. What the hell?? Life is the longest damn thing anyone ever does!! What can you do that's longer?




9
 When you are waiting for the bus and someone asks 'Has the bus come yet?'. If the bus came would I be standing here, dumbass? 

 

If you are having a bad day, remember it could be worse...

If you are having a bad day,  remember it could be worse...