Monday, February 15, 2010

Ngwasuma ngwasuma ngwasuma...

Mambo gani ya kuweka mikoni kwenye kiuno wewe? Unafikiria hii ni Bongo eeh? Kaa chonjo hiyo miondoko yako inaweza kuleta braah kwa watu wengine. Mdau anafurahia starehe ya bure huyu. Hapa akiamka ndiyo atajikuta anajuta kwani "MAKARATASI" yalipiga simu kwa sana na kuamua kurusha vijishati vyake nje ya mlango...Akirudi nyumbani ataelewa nini maana ya CURFEW huyu!

Hii inatia uzuni kwa kweli!

Sasa unataka kuniambia kwamba kweli hapa kuna umoja jamani? Wewe kama unaweza kula bata Monday hadi Sunday na unajua kuna watoto kama hawa wanahitaji msaada basi lazima uje kuwa "KUNI" motoni nakwambia. Mimi siwezi kuamini kwamba mtoto mdogo kama huyu ataweza kufika mbali kiuchumi kwani mgogo wake hadi hapo tu utakuwa umechoka mbaya na unaniambia aende shule ana afaulu shule ya msingi. Serikali yetu inabidi kuweka mitihani tofauti kidogo kwani kwa wale wanaotaabika kwenda shule basi wapewe kiji"favor" bwana!

Friday, February 12, 2010

Kibao kipya kinachovuma pale nchini Ethiopia!

Asikwambie mtu kibao hichi ni balaa kwa sasa na kinatamba sana kila kona ya nchi hiyo. Mwimbaji wake alikuwa ni Engineer wa Cornejo & Sons anakwenda kwa jina la Msukuma a.k.a Buluba. Unaweza ukakipata kibao hivi kama uki"log in" kwenye youtube.com. Title ya song hili ni "FUMBA MACHO" na ndiyo maana kila mdau hapa amefumba macho yake. Big ups kwa producer na writer wa song hilo ambaye anakwenda kwa jina la DJ Dula...Thanks a lot pal!

USIKU UNA MENGI MWANAWANE!

Mkali wa miondoko ya Rap nchini Marekani pichani kulia akiwa anaweka mambo ya after party safi. Mdau huyu bwana ana mke lakini naona kama pete ya ndoa ipo kwenye kidole tofauti vile au ni macho yangu tu? Halafu mbona shati limechomoka kwa mbele peke yake? Kunani pale mtu wangu?

Hii ilikuwa ni shughuli kwa kweli sasa wacha nijikalie kimya mtu wa watu mie nisije kajasutwa bure! Tehe tehe!

Hii kiwanja ni Child Abuse kabisa!

Hakuna kosa ambalo mwanafunzi wa shule ya msingi anatakiwa kuadhibiwa kama hivi bwana. Hapa unaweza kusema kuwa mwanafunzi atajifunza kweli kutokana adhabu kama hizi? Mwangalie huyu wa nyuma kwani hata shoes hana amejitahidi kweli kuja kufuta ujinga but mwalimu bado haoni hilo na kuendelea kumhadhibu...Mimi roho inaniuma kweli nikiona mambo kama haya hasa hasa yanatokea kwenye nchi za joto kama zetu kwani hapa hakanyanyuka huyu mtoto jasho mwili mzima na hewa nzito ya kumfanya mtu awe bubu for a while!

BONGO NGOMA HAITAISHA...

Sasa picha kama hii jamani inamaanisha nini? Hizi picha huwaga naziona kwenye website za watu wazima tu na sasa naona zimeanza kuingia bongo.(BONGO KUNANI) Dada umependeza mwayego kwani huo ni mkanda sijui au ni chachandu za kisasa.... yenye rangi nyekundu, imepita mahala pazuri kweli...muwashowasho huo...Umeona hiyo wewe Pierre "Kabumbu"?

WAPO WAPI HAWA?

Bongo kuendeleza fani ni kazi kwani matapeli wengi sana. Vijana walikuwa on fire kipindi kile cha kale ila baada ya kuwika bila mafanikio sasa sijui wamejichimbia wapi. Baadhi yao sasa hivi wapo hapa kwa baba Obama wanakula BATA as always. Mdau wa nyuma amekamata weusi kwa kwenda mbele, jua la bongo noma ila kwa sasa msela huyu yupo USa upande wa Mashariki kule karibia na Madson Square kaiva hivi....anaonekana kama " POINT FIVE"

Miss Mtwara Remix...

Ericka Mchatta pichani kulia...siamini amekua mmama hivi kweli tunda baya. Enzi za nyuma kisura alikuwa MVP kwenye mambo ya urembo ona sasa hivi....Daaamn hujafa hujaumbika kwa kweli! Kutoka kuwa kama Alicia Keys mpaka kuja kufanana na Busta Rhymes!

Thursday, February 11, 2010

Mambo gani sasa haya tena?

Kama kula tunda huwezi basi acha mwanawane. Sijui ni umri ndiyo umefikia pabaya au ni tatizo jingine kwani kijana aliangusha kwa muda mrefu bila hata kujifahamu. Chauka kuna Pobobawa kwangu so be careful! Hilo lilikuwa ni wazo la bure tu na ni warning kwako kwani siku nyingine unaweza ukaamka na mabaki ya yai bichi kwenye makalio.

Hii picha kapiga nani?

Wewe unampiga picha mwanamke kwenye kitanda akiwa ameshika kilaji...ulikuwa una maana gani? Dada huyu bwana kapendeza kweli na anaonekana wala halikuwa hana ihana na mtu kwani kajitulizia mkiwa wake kwenye kitanda cha Guest za Kimara. Lazima hapa utoke na mba kwani panaonekana kabisa kuwa hapafai mwanawane. Ila shemeji hoteli ya mtoto imependeza kweli...so tasty! Yummy yummy...

Jamani ni kiwanja kweli hapa?

Yaani kweli Bongo kuna mengi kwani watu wanakula "BATA" na ndala? Sasa kama wewe unakwenda kula tunda na hata huwezo wa kununua viatu tu huna unataka kuniambia kwamba una akili kweli? Ukikanyagwa je? Ndiyo maana nyapu za Bongo kucha mbaya kwani ni kwasababu ya kukanyagwa sana Kiwanja! This needs to stop!

Majani mabaya!

Mdau Ngassa D akiwa na Baba Naima...hapa inaonekana faza wa kushoto yupo majani si kitoto, na hiki kijiti nadhani ni cha Newton, Kansas kwani tapeli huyu hupenda sana kuhudhuria places hizo. Ngassa D nayeye anaonekana alikuwa ameshiba kweli maana alivyosimama tu basi utagundua kwamba Mpemba huyu alikuwa amevimbiwa!

Nguza, Papii kurudi gerezani kutumikia kifungo.

MAHAKAMA ya Rufaa nchini imeamuru mwanamuziki Nguza Vikingi na mwanae Johnson Nguza warudishwe gerezani kwenda kutumikia kifungo cha maisha baada ya kuonekana kuwa na hatia ya kutenda makosa hayo.

Mbali na wawili hao kurudishwa gerezani mahakama hiyo imewaachia huru watoto wa mwanamuziki huyo ambao wote walikuwa wanatumikia kifungo hicho baada ya mahakama hiyo kuona washitakiwa hao walibambikiziwa kesi.

Walioachiwa huru ni mshitakiwa wa tatu Mbanga Nguza na mshitakiwa wa nne, Fransic Nguza ambao ni watoto wa mwanamuziki huyo wameonekana kutokuwa na hatia na hawakuhusika katika ubakaji huo.

Nguza na Johnson “Papii” wamerudishwa gerezani kwa kupatikana na mashitaka matano ambayo yaliwarudisha rumande kati ya mashitaka 23 yaliyokuwa yanawakabili awali.

Hivyo hukumu hiyo ilioyotolewa mahakmani hapo leo asubuhi ndio mahakama ambayo ina mamlaka ya mwisho dhidi ya rufaa iliyowasilishwa na washitkwia hao na hawataweza kuachiwa huru tena labda msamaha wa rais uweze kuwakomboa wanamuziki hao.

Tuesday, February 9, 2010

Yanga Yaivurumisha Mtibwa.

Krosi safi ya John Njoroge katika dakika ya 15 ilimfikia Boniface Ambani aliyeukwamisha mpira kimiani huku kipa Shaaban Kado asijue la kufanya, bao hilo lilidumu hadi katika dakika ya 30 baada ya Mohamed Ally wa Mtibwa kusawazisha bao hilo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Bao la pili la Yanga lilifungwa na Steven Bengo katika dakika ya 84 na dakika sita baadaye, Geoffrey Bonny aliifungia Yanga bao la tatu kwa shuti kali nje ya 18.
Kwa matokeo hayo, Yanga imefikisha pointi 36 huku Simba yenyewe ikiwa na pointi 43 ikiwa ni tofauti ya pointi saba.

Jah Kimbute feat. Kajumulo...

Hapa kazi ilikuwepo...mwangalie Baba Chuki kulia picha na mdogo wake Baba Naima...wameacha familia zao nyumbani na sasa wanamwaga radhi tu. Namuonea huruma sana mrembo huyu kwani ni bora akae mbali na hii combination ya Chamriho ni wabaya sana kwa pasi fupi..."KURA URIWE" ndiyo style yao wadau hawa!

Mrembo wa week!

Kazi ipo...sasa jamani kama unaishi na presha kama hii nyumbani si ni bora niwe na mganga wa kujitegemea? Kwani nitakufa kwa Heart Attack mapema sana may be baada ya Honey moon. Kuna watu wameumbwa halafu kuna wale walio umbwa kwa more than normal days! Huyu naona walimuumba siku ya nane na ya tisa. (DIAGI JANGUO) Daaamn girl you are hot!

Sometimes ndoto nyingine ni Impossible kuwa kweli!

Dogo anaonekana kuanza kukata tamaa kwani nauhakika kabisa hilo guitar halitoi sauti kabisa. Huyu kilichobakia ni kuacha shule na kuanza kuvuta "NDUMU". Mdau wa kulia sijui anafanya nini kwenye photo hii. Wazungu bwana...wamewatandika picha watoto hawa kwenye banda sijui...I'm mad for real! Ila wee Ronald si ukamchukue mdogo wako mwa mwisho huyu kule Lindi basi? Usimwache kama hivi bwana...mnunulia hapa payless shoes basi na yeye aonekane ana bro kiwanja mwanawane...

Tumetoka mbali jamani...

Unaniambia niisaidie Haiti na wakati tulipotoka tu ni kama motoni! Kweli hapa unategemea mwanafunzi awe na mwandiko mzuri kweli? Mambo mengine mimi yananiumiza moyo kweli kwani nikiona hivi halafu huku ng'ambo watu wanakula "BATA" ...Ila Mungu mkubwa kwani ndiyo maneno ya watu masikini kama wakina sisi. Kila mara tukiishiwa basi tunasema "MUNGU YUPO" Hii ni shule ya msingi ambayo mdau wetu Salehe a.k.a Kanye West ndiyo alikuwa Kiranja mkuu kwa muda wa miaka miwili kabla ya nafasi hiyo haijachukuliwa na Mwesiga a.k.a Tolu!

Gari moshi Chiboko!

Mwandisi wa kujitegemea "Msukuma" mbeleni kulia akiwa anaelekea kwao Magu few weeks ago wakati alipokwenda kutembelea Bongo baada ya kupata shahada yake ya Uhandisi katika Chuo Kikuu cha Wichita State. Mdau huyu alikuwa analala kwenye Motel ya Kashozi Inn pale Magu, Mwanza. According na yeye ni kwamba alikuwa ana"share" kitanda na mtu mwingine kwani Motels wilayani hapo ni moja tu...Sasa swali langu kwake lilikuwa ni " Walikuwa wanatumia shuka moja na je walikuwa wanalala na boxers and chupi tu" Alishindwa kabisa kunipatia jibu la swali langu na alionekana kuchefukwa sana kwa swali hilo....Anyway nitamuuliza sometimes this month!

Monday, February 8, 2010

Uingereza Kuzibania Viza Za Wanafunzi.


Serikali ya Uingereza imetangaza kuweka sheria na masharti magumu katika utolewaji wa viza za uanafunzi.Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza, Alan Johnson ameiambia blog hii kuwa masharti magumu yameongezwa katika maombi ya viza za uanafunzi kwa wanafunzi toka nchi zote duniani.

Mojawapo ya masharti yaliyoongezwa katika uombaji wa viza za uanafunzi ni kwa mwanafunzi anayeomba viza kutakiwa awe anaongea kiingereza fasaha.
Miongoni mwa sheria ziliongezwa ni kama vile kuwazuia wanafunzi wenye viza za muda mfupi kuwaleta Uingereza jamaa zao kama vitegemezi (dependant) wao.

Sheria mpya zimewekwa kufuatia waziri mkuu wa Uingereza kutaka masharti ya utolewaji wa viza yaangaliwe upya kufuatia tukio la mwanafunzi wa Nigeria aliyemaliza masomo yake nchini Uingereza kujaribu kuilipua ndege ya Marekani bila mafanikio. Sababu kubwa ya kuwekwa kwa sheria hizi ni kupunguza idadi ya wanafunzi toka barani Afrika na Asia ambao hujishughulisha zaidi na kufanya kazi kuliko masomo yao.

Awali mwaka mmoja uliopita Uingereza iliongeza ugumu katika utolewaji wa viza za wanafunzi kwa kuwataka wanafunzi watoe vithibitisho vya kuweza kujilipia ada yote ya masomo yao na pia kuwa na uwezo wa kifedha kukimu gharama za maisha yao nchini Uingereza. Wiki iliyopita, Uingereza ilisimamisha kwa muda kupokea maombi ya viza za wanafunzi kutoka maeneo ya kaskazini mwa India, Nepal na Bangladesh. Hatua hiyo ilitokana na idadi kubwa kuliko kawaida ya maombi ya viza za uanafunzi toka maeneo hayo.

Wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza imesema kuwa kutokana na masharti mapya ya utolewaji wa viza za wanafunzi, idadi ya wanafunzi watakaopewa viza itapungua sana lakini hata hivyo wizara hiyo ilikataa kutoa tathmini zao.

Nyangombori Remix 2010.

Goose alianguka...Mwanawane hii team inatisha kwani ilinza kula bata since morning mpaka morning na bado vijana walikuwa wanaliendeleza. Ila machizi wangu Bongo lini? Kwani naona mmeamua kuacha kwenda kusalimia wazazi nyumbani kwenu huko Vigwaza, Kibaha.



Matapeli hawa waliamua kumtimua DJ na kuanza kupiga live musics. Msanii wa kujitegemea Stanboi "The African Child" kulia akiwa ready kuturusha. Huyu Baba Chuki na matambaa tambaa yake kama "SAGAJIWE" lililotoka Iringa bwana. Next time nitampa na shuka kabisa alivae basi...tehe tehe tehe!


Wow...jamani mtoto ana "DOMO" zuri huyu...Jicho la maana na nyweli zilizokwenda kuchukua CPA na siyo wig kama za baadhi ya dada zetu. Ehe he he yule si mdau Rama? Anafanya nini tena sasa? Kweli usiku una mengi...Stanboi be careful kwani Baba Chuki anapenda magoli ya kuvizia huyu...ask me I know him better!


King Kupaz kavua hadi shati...mmh kazi ipo hapa. Mtoto anabahati sana hapa ilikuwa ni kwangu kwani kama si hivyo basi we would be talking about Child Support and stuff if you know what I mean.



Tapeli la Kibantu limetulia na karatasi. Mdada ana rangi ya kutia kama PERA. Hapa najua kila mtu anajidai kuwa yupo single ila hataki uende kwake...unajua hiyo ina maana ya kwamba kuna mtu anaishi naye. Hii story lazima niifuatilie kwani iko very interesting especially to my viewers.

Twendeni shule jamani...

Unafanya utani na Pombe...utaharisha. Tapeli Baba Chuki anaanza kuangusha taratibu...kijana amependeza ila sasa hii jersey inaonekana kama siyo yake kwani ni ndefu sana sehemu za mikononi.I'll ask him next time nakutana naye.


Kijana Eilmer na matapeli wa Wichita, Pierre kulia na Aaron kushoto wanaonekana wakimpongeza kamanda huyu kwani ana less than a week kuwa deployed Afghanistan ready for a real battle. Kila la heri SSG Eilmer Nkomo. "Acha kuzaa huko kwani wengi wenu nimesikia mmewazalisha sana watoto wa Kiarabu"


Hivi huyu jamaa anaona kweli? Tungi baya maana mdau kama huyu...unaweza kumkuta anakwambia bado yupo safi kuendesha gari na wakati hata kufumbua macho tu ni mtafutano...


Damn...sasa hii sijui ilikuwa ni kucheza mziki au ni mambo ya kinguonguo maana hii position iliyokuwa hapa ni balaa tupu. Chauka "KURA RAHA" maisha mafupi haya mpwa...

Kiwanja kitamu bwana...

Hii ilikuwa kwenye basement yangu...Vijana walikula BATA hawa acha mchezo. Hapa ilikuwa ni mishale ya kumi na unusu ya majogoo...



Mambo ya faranga bwana kwani tuliweka DJ wa kike kuturusha...Thanks to Mama Kunta kwani alitudundisha ma "Masotoo" ya enzi hizo za kina Bozi Boziana...kibao cha Tembe na Tembe kilinifanya nikumbe Home kabisaaa....



Nilimlipa DJ Smilez ili kutumbuiza vijina but it didn't work right kwani kijana hajazoea kuona leather coaches kama hizi. Ilimchukua few minutes tu kuanza kusinzia na kuacha sherehe inamsubiri azinduke...


Mdau analamba tungi huyu never seen before...hapa alikua ameanza na bia ya kijana ila hadi tunakaribia mishale ya morning alikuwa na bia ya Budweiser...Hadi tunakwenda mitamboni tapeli huyu alikuwa anaumwa vibaya sana....Pombe za bure ni sumu.

Friday, February 5, 2010

Bwana weeeh...

Angekuwa kiwanja huyu...basi hasingeliona jua for a very long time kwani so far nimeshaziona kama tickets 32 na zote ni lazima kwenda kumuona jaji. Mmmh...Bongo kweli hakuna safety kabisaaaa. Hata kama hii style wanaiita "mshkaki" ila hapa nadhani wanatakiwa kuuita pilau kwani kila kitu kimewekwa ndani na haina haja ya mboga wala nini! Sijui hawa watoto ni wake au la hasha! Let me leave him alone kwani kila mtu anajikuna kwa urefu wa mkono wake mwanawane...

Tapeli la week!

Tapeli wa kujitegemea, Martin Elia a.k.a Jump Around...nimekukubali mpwa kwani unakula "BATA" kwa mzee George Washington na vile vile unaliendeleza kwa Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere. That's what I call...enjoying yourself! Huyu cameraman hakunifirahisha, alitakiwa kupiga hii picha kwa mbali zaidi ili niweze kutoa marks kwa mdada huyu hapa kwani so far amepata maswali 23 kati ya 35 ila kumi yapo section B "USAFIRI" na hapa siyaona majibu bado...so next time mdau remember kuchukua picha better enough to get the results!

Mambo gani sasa haya tena?

Mdau wa kulia pichani kweli ni mlevi, kwani huwezi kulea kwa kiasi hicho na kuendelea kuing'ang'ania lager kama vile! Pombe za mchana zina mengi....Huyu mdau wa kushoto nadhani ni mlinzi na sasa anauchapa usingizi kwasababu ya uchovu wa kuwa macho usiku mzima. Hivi unaweza kunisaidia kunipa idea "why" huyu mdau wa kulia ameurusha ulimi wake nje? I was thinking kwamba jamaa anakula nzi kwasababu Bongo kuna nzi wengi na wanakuwa wakubwa kama mbung'o...

Hapa ndiyo kiwanja wewe....

Wewe umeona nchi gani dunia rais anafanya mambo kama haya? Ni US tu pekee. Kweli huku ni kama kuishi zama za Yesu ukiwa Israel yaani unakuwa unakula tunda tu, the only thing you need to do ni kujiunga na msafara wa Yesu basi unatandika menu. Kwanza Janitor kapiga "MTI" chini...Wow! Maisha haya unipeleke popote kule may be kwenda home Bongo tu kusalimia ndugu, jamaa na maadui...Amen!

Jamani hii sasa ni SOO!

Jamani kweli hapa si ni pesa tu? Mzee anaweza kufa na heart attack huyu na bintiye wa mwisho naye wala haogopi kufanya kitendo hiki. Mimi naona kuwekwe umri wa mwisho wa kufanya mampenzi. Mshua amechoka kweli kweli kwani jasho linamtoka kwa kwenda mbele, mimi naona hii style haikumfaa kabisa hasa hasa ukizingatia umri wake ni wa kuwekwa Nursing Home! Ghetto limechoka kinoma, angalia TV na stand yake....damn! Huko ahera kutakuwa na hukumu za ajabu sana, I can't wait!

Wednesday, February 3, 2010

Mwanafunzi Aiuza Bikira Yake Kwa Dola 32,000.


Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 19 aliinadi bikira yake kwenye mtandao wa www.ineed.co.nz baada ya kukabiliwa na ukata wa pesa.

Mwanafunzi huyo anayejiita "Unigirl" alijitambulisha kuwa yeye ni mrembo mwenye kuvutia, yuko fiti na mwenye afya njema.Zaidi ya watu 1,000 walijaribu kuinunua bikira yake lakini mwanaume mmoja ambaye hakutajwa jina lake aliibuka mshindi baada ya kuweka dau kubwa la dola 31,900. (Takribani Tsh. Milioni 42).

"Nawashukuru watu wote zaidi ya 30,000 waliolitembelea tangazo langu, na zaidi ya watu 1,200 walioweka madau yao kuinunua bikira yangu", alisema mwanafunzi huyo."Dau lililoshinda ni kubwa sana kuliko hata nilivyotarajia".

Mwanafunzi huyo alisema kuwa hajawahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na pesa atakazopata atazitumia kulipia masomo yake.
Mwanafunzi huyo aliendelea kusema kuwa ili mradi masuala ya afya yake yatapewa kipaumbele hana hiana kumtunuku bikira yake mwanaume yoyote yule bila kubagua kabila wala umri ilimradi apate pesa za kulipia masomo yake.

Mmiliki wa tovuti iliyotumika kuinadi bikira hiyo, Ross MacKenzie, alisema kuwa tangazo la mwanafunzi huyo lilikuwa ni halali kisheria na hakuna sheria yoyote iliyovunjwa.Mwanafunzi huyo aligoma kufanya mahojiano na waandishi wa habari lakini MacKenzie, aliliambia gazeti la Waikato Times kuwa ameruhusiwa kutaja kiasi cha dau lililoshinda bila kutoa maelezo ya ziada.

Matukio ya wanawake kuzinadi bikira zao kwenye internet yaliibuka kwa kasi baada ya mwanafunzi wa Marekani Natalie Dylan ,22, kuinadi bikira yake na kupata mteja aliyeweka dau la dola milioni 3.7.Natalie naye wakati anainadi bikira yake alitoa sababu kama hizi kuwa anatafuta pesa za kulipia masomo yake.

Mwezi mei mwaka jana nchini Ujerumani, mwanamke mmoja toka Romania, Alina Percea, 18, aliinadi bikira yake kwa matumaini ya kuingiza mamilioni kama Natalie lakini aliambulia euro 10,000 tu toka kwa mfanyabiashara wa Italia mwenye umri wa miaka 45 aliyeshinda katika mnada huo.

Mbali ya kupata dau dogo, Alina alipata hasara zaidi baada ya maafisa kodi wa Ujerumani kuzikata kodi pesa alizopata kwa kuinadi bikira yake akiambiwa kuwa alichofanya ni sawa na wanachofanya makahaba ambao nao wanalipa kodi kwa shughuli zao.

Alina alibakia na karibia nusu ya pesa alizopata baada ya makato ya kodi kufanyika.

Acha uchoyo mpwa!

Damn kweli kuna watu wana roho ngumu! Mdau anaomba plate ila inaonekana kama anapewa napkin.... Ebwana eeh wabongo nuksi. Ila mdau inaelekea kuwa ameridhika na jibu alilopewa kwani naona ana"smile" kabisa bwana. Nafikiri "may be" ni kwasababu camera ilikuwa usoni sasa sijui nje kuliendelea nini....Let me check with my assistant and obtain more details about what really happen at the end of this tukio...TO BE CONTINUED!

Kura Uriwe!

Huyu jina kwa kifupi ni Muchunguzi Rugaimukamu Rutashobya Buberwa Rwechungura Mulokozi Mushumbuzi Rwegasira a.k.a Chidi Benzi. Yeye ni mwenyeji wa Lushoto, kule mkoani Tanga. Anapenda misosi mdau huyu, kwa kweli nimemkubali kwani ni kama MVP kwenye matukio yanayohusisha menu. Anyway...ona kijana aliyeinama eti anaikimbia camera ya paparazzi, sasa wewe unajua kabisa kuwa jacket lako tu linakujulisha kuwa wewe ni nani, basi vua nguo tusikujue kabisa....Pumbafu weee! Nyan'gau mkubwa! Tandarubeta wa masika...tehe tehe tehe!

Mtoto wa Nyoka ni Chura...

Unaouona mguu wa dogo ulivyojikunja? Unataka kuniambia ni nini hasa kilichofanya dogo akunje mguu huyu? Mmmh Duniani kuna mengi jamani...Anyway tuyaache haya bwana kwani motoni kila mtu atakwenda kwa fair yake!

Tuesday, February 2, 2010

MSIBA WA MTANZANIA MWENZETU...

Kwa habari zilizotufikia katika meza yetu ya blog ni kwamba, mwenzetu na mwana"community" mwenzetu John Tesha (Kulia) pichani na dada yake Jema Tesha (Hayupo pichani) wamefiwa na baba yao mzazi. Kama ilivyokuwa tamaduni zetu waafrika, tunawaomba sana kujitokeza kwenda kuwapa pole ndugu zetu huwa.

Kwa more details basi unaweza kufungua website ya tawicha.net au wasiliana na mfiwa John Tesha kwa namba hii:

John Tesha (JT): 316-371-3866.

Monday, February 1, 2010

Nadhani kilichofuata ni TIFU!

Ingekuwa kama ni wewe ungefanya nini hapa? Maana kwa kweli inaonekana kama washkaji hawa wanamapenzi ya makaratasi kama wengi wetu tulivyo huku. Kwani inabidi ukubali matokeo tu no matter what the circumstances are...au wewe mdau Munis unacomment vipi hapa? Thanks!

Mmmh...mimi hapa siamini kabisaaaa...

Huyu naye kinamchekesha nini sasa jamani? Huwezi kunywa hiyo bia ya watulivu na kuanza kumwaga lazi kama hizi bwana! Nadhani alichukua hicho kinywaji kwa mdau wa nyuma pale ili apige nacho picha. By looking at this photo, unashtukia kabisa kuwa mdau huyu alikuja na VISA ya visiting. I don't wanna write much kwani wanaweza kuni"sue" bure. Mwanamke wig bwana!

Mademu wa Kibongo hawaaminiani kabisa...

Dada kaona hapa kilaji mdau kakichapa lazima aende nyumbani na mimi kwani, yasije yakawa mambo ya "Blame it on the a-a-a-a-a alcohol". Angalia shati ilivyovyutwa yaani kweli hii ni braah! Kuna njemba upande wa kushoto pale akiwa ana vazi la Jersey za Walmart, nadhani alikuwa anazomea floor yule. Lager za bure hizi zinarudigi mida mibaya sana mwanawane!

Togo Wafungiwa Kushiriki Mashindano Ya Afrika...

Mmoja wa mwili ya waiouwawa katika timu ya Togo na waasi.

Halmashauri kuu ya CAF imeifungia timu ya Togo kwa uamuzi wake wa kujiondoa kwenye michuano ya Afrika huko Angola. CAF iliona kitendo hicho cha CAF kujitoa kwenye michuano hiyo ni cha kisiasa zaidi, hii ni sababu wachezaji walikuwa wako tayari kushiriki. Uamuzi huu unaifungia Togo katika michuano ya Afrika ya mwaka 2012 na 2014.

Mpaka sasa watu wengi wamekasirishwa na uamuzi huwo wa CAF kwa kutozingatia hali halisi ambapo watu watatu wa timu ya Togo waliuwawa siku mbili tu kabla ya michuano hiyo kuanza.

Sebene inapokolea...

Karatasi hili...limemuacha mdau anapiga double ya kubeba wazee kazini halafu yeye kawaita marafiki wake na kwenda kujimwaga kwenye starehe. Hapa bwana lazima ukubali matokeo kwani navyowajua wabantu mimi...hili karatasi halina muda mrefu litakushinda tu. Ila nachowashukuru Wabongo wenzangu ni kwamba, wengi wao ni wavumilivu kweli kwani ndiyo hali halisi ya kupata kibanda cha karatasi...au wewe Martin unaniambiaje?

Aisha Madinda mwanawane...

Daah....ndiyo maana Bongo UKIMWI umezagaa sasa kweli jamani unataka kuniambia umezichapa lager za maana na umepitiwa mbele na jimama kama hili, then likaomba lift na kutaka umsaidie kumlipia chakula...kweli mwanawane unataka kuniambia utakataa ofa ya kwenda kumaliza kiu? Acha habari yako wewe... Maisha mafupi bwana kama ukipata ngoma ni kama kupinduka kwenye Bajaj tu.

That's not her food....

Sasa niambie kama wewe unaweza ku"handle" jimama kama hili? Acha mchezo bwana kuna magari mengine yametengenezwa ili yasiendeshwe na watu ni kwa ajili ya maonyesho kama sabasaba vile. Hapa hakinyanyuka lazima kila mtu amtazame bwana kwani ni one in a million kuona makalio kama haya duniani.

Mambo ya kawaida jamani...

Kama unaona kuwa kuna kitu kinakufurahisha humu kwenye blog yangu basi hakuna noma kama ukiniangushia sifa mwanangu mwenyewe.....
Washkaji Mungu akipenda tutaonana basi.........ila kumbuka kuwa Mungu ni mmoja na siku zote anafanya maajabu kwahiyo si mbaya kama tukimshuru kwa kila nia.....
Mungu awabariki watu wote wa Dunia hii.Amen!

9 Things I Hate About Everyone

1. People who point at their wrist while asking for the time.... I know where my watch is pal, where the hell is yours? Do I point at my crotch when I ask where the toilet is?



2
 People who are willing to get off their ass to search the entire room for the T.V.. remote because they refuse to walk to the T.V. and change the channel manually. 

3
 When people say 'Oh you just want to have your cake and eat it too'. Damn right! What good is cake if you can't eat it? 

4
 When people say 'it's always the last place you look'. Of course it is. Why the hell would you keep looking after you've found it? Do people do this? Who and where are they?   cause I amGonna Kick their asses! 

5
 When people say while watching a film 'did you see that?'. No Loser, I paid $12 to come to the cinema and stare at the damn floor. 

6
 People who ask 'Can I ask you a question?'.... Didn't really give me a choice there, did ya sunshine? 


7.
 When something is 'new and improved!'. Which is it? If it's new, then there has never been anything before it. If it's an improvement, then there must have been something before it, couldn't be new.

8
 When people say 'life is short'. What the hell?? Life is the longest damn thing anyone ever does!! What can you do that's longer?




9
 When you are waiting for the bus and someone asks 'Has the bus come yet?'. If the bus came would I be standing here, dumbass? 

 

If you are having a bad day, remember it could be worse...

If you are having a bad day,  remember it could be worse...