yake kwa jina la kitaalamu hujulikana kama
"Uumbuajiasis Viongozitanzanialitis Hadharanum."
Ugonjwa huu unatokana na kufuatilia mambo ya serikali na
viongozi kwa karibu kiasi cha kutaka kuweka ubovu wao hadharani.
Dalili kubwa za ugonjwa huu ni hizi:
a. Kupenda nchi zaidi kuliko chama
b. Kuwa tayari kutetea mali ya Taifa na kuilinda mali hiyo
c. Kutoogopa yatakayokukuta
d. Kuanza kuweka hadharani ubovu na siri za viongozi hasa kwa jamaa
yako karibu
e. Kutosikiliza ushauri wa kutakiwa kukaa kimya na wakubwa wako
f. Kuwa kimbelembele kuzungumza na kukemea maovu kila upatapo nafasi
g. Kuwa mtetezi wa Katiba na mkosoaji wa jamii
h. Kutolegeza msimamo hadi kifo.
Maambukizi:
Ugonjwa huu unaambukiza watu wachache kwani watu wengi wameshapatiwa
kinga yake. Kwa wale wanaombukizwa wanafanya hivyo zaidi kwa kusoma habari za ufisadi, rushwa, na ubadhirifu katika serikali yao . Kwa kupitia
mitandao, vitabu, na vyombo vya habari , virusi vya ugonjwa huu vinajipenyeza katika akili za watu na kusababisha kusisimka kwa ubongo.
Wale waliombukizwa ugonjwa huu hujikuta wakitafuta habari za kila namna
na kushiriki mijadala yenye kutafakari mustakabali wa Taifa lao.
Kinga:
Ugonjwa huu kinga yake kubwa hujulikana kwa kitaalamu kama Mlungura.
Kinga hii hutolewa kwa wale wote wenye kuanza kuonesha dalili za kukumbwa na ugonjwa huu.
Kinga hii huwekwa kwenye mabenki na maofisi
mbalimbali ili kuzuia viongozi wakubwa wasipatwe na virusi vya
ugonjwa huu. Kinga hii pia hufanya kazi kwa wale walioanza kuonesha dalili kama kina Zitto, Marmo, Mzindakaya, Slaa, Rev. Mtikila n.k
Pindi mtu akishapatiwa kinga hii
HAWEZI kuipinga serikali!
Tiba:
Hadi hivi sasa ugonjwa huu hauna tiba ya uhakika kwani wale ambao
wameshaugua kwa muda mrefu hawako tayari kutibiwa kwani wanaona
wanaishi vizuri tu na ugonjwa huu.
Karantini:
Pindi baadhi ya wakubwa wakiona kuna mtu ambaye amefikia hatua ya
juu kabisa ya ugonjwa huu basi kwa mbinu wanazozijua wenyewe
wanamkarantini, na wakati mwingine anakuwa katika hali hiyo ya
kutengwa hadi kifo ili asiendelee kuwaambukiza watu wengine.
Jihadhari:
Kwa vile ugonjwa huu ni wa hatari, watu wabadhirifu, wezi wa mali ya
umma, walaghai, na mafisadi hawawezi kuustahimili.
Ugonjwa huu ni kinyume kabisa na watu hawa hivyo kama hutaki kuambuzizwa hakikisha unaendelea
kujikita katika katika vitendo viovu vya kuharibu mali za umma na
kuivunja vunja nchi huku ukishiriki katika kumegeana hazina ya
Taifa.
Kwa vile ugonjwa huu unaendelea kuambukiza taratibu, kuna
kila dalili hapo ulipo UNAISHI NA MWATHIRIKA!
Zinduka, Kapime ujue afya yako ugonjwa huu upo