
Krosi safi ya John Njoroge katika dakika ya 15 ilimfikia Boniface Ambani aliyeukwamisha mpira kimiani huku kipa Shaaban Kado asijue la kufanya, bao hilo lilidumu hadi katika dakika ya 30 baada ya Mohamed Ally wa Mtibwa kusawazisha bao hilo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Bao la pili la Yanga lilifungwa na Steven Bengo katika dakika ya 84 na dakika sita baadaye, Geoffrey Bonny aliifungia Yanga bao la tatu kwa shuti kali nje ya 18.
Kwa matokeo hayo, Yanga imefikisha pointi 36 huku Simba yenyewe ikiwa na pointi 43 ikiwa ni tofauti ya pointi saba.
No comments:
Post a Comment