Mwanamke mmoja nchini Japan amewashtua watu wengi nchini humo baada ya kukiri kuwa alikuwa akimuosha mtoto wake wa kike wa miaka mitano kwenye mashine ya kufulia nguo ili kumfundisha adabu.
Junko Egashira mwenye umri wa miaka 34 aliwaambia polisi wa magharibi mwa Fukuoka nchini Japan kuwa mara kadhaa alikuwa akimweka mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka mitano kwenye mashine ya kufulia nguo na kisha aliiwasha mashine hiyo. Mwanamke huyo alisema kuwa alikuwa akifanya hivyo ili kumtia adabu mtoto huyo anapoleta utundu. Junko aliwaambia polisi kuwa alikuwa akiifunga pamoja mikono na miguu ya mtoto wake na kuuziba mdomo wake kwa kutumia gundi ya platiki na kisha kumweka ndani ya mashine ya kufulia nguo na kuiwasha mashine hiyo kwa dakika kadhaa. Katika mojawapo ya mateso ambayo Junko alikuwa akimfanyia binti yake ni kuifunga mikono yake kwa kamba na kisha kumweka mtoto huyo ndani ya ndoo iliyojaa maji. Mtoto huyo alifariki dunia juni 27 baada ya mama yake kumfunga kamba shingoni na kisha kumning'iniza ukutani. "Nilimfunga kamba shingoni na nilimning'iniza ukutani baadae nilimkuta amefariki, sikufikiria kama angefariki", Junka aliwaambia polisi. Junka alianza kuishi na binti yake huyo miaka miwili iliyopita baada ya kutengana na mumewe. Junka anakabiliwa na mashtaka ya mauaji. | ||
| ||
|