Halmashauri kuu ya CAF imeifungia timu ya Togo kwa uamuzi wake wa kujiondoa kwenye michuano ya Afrika huko Angola. CAF iliona kitendo hicho cha CAF kujitoa kwenye michuano hiyo ni cha kisiasa zaidi, hii ni sababu wachezaji walikuwa wako tayari kushiriki. Uamuzi huu unaifungia Togo katika michuano ya Afrika ya mwaka 2012 na 2014.
Mpaka sasa watu wengi wamekasirishwa na uamuzi huwo wa CAF kwa kutozingatia hali halisi ambapo watu watatu wa timu ya Togo waliuwawa siku mbili tu kabla ya michuano hiyo kuanza.
No comments:
Post a Comment