
Charl Van den Berg, 28, shoga toka Afrika Kusini aliwafunika mashoga wenzake toka Australia, Hong Kong, China, Tanzania na Hispania na kutwaa taji la dunia la kumtafuta mwanaume shoga mrembo kuliko wote duniani kwa mwaka 2010. Charl ambaye anaendesha mgahawa wa chakula mjini Cape Town nchini Afrika Kusini alitwaa taji hilo baada ya mashindano ya siku nne ya kuvaa mavazi mbalimbali yakiwemo mavazi ya kuogelea.
Taarifa ya waandaaji wa mashindano hayo ilisema kuwa dhumuni kubwa la mashindano haya ni kumtafuta mtu atakayekuwa kiongozi wao katika kutetea haki za mashoga duniani. Xiaodai Muyi, 26, shoga toka China alishiriki na kushika nafasi ya nne katika mashindano hayo pamoja na hatua za China kumzuia asishiriki mashindano hayo.
Mamlaka za China ziliyapiga marufuku mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa China katika mashindano hayo. Xiaodai aliingizwa kisiri kwenye mashindano hayo ambayo wanaume 20 toka nchi mbali mbali duniani walishiriki kumtafuta mrembo baina yao. Ushoga ulikuwa ni kosa la jinai nchini China hadi mwaka 1997 wakati sheria zilipobadilishwa na kuwahesabu mashoga ni watu wenye matatizo ya akili.
Raia wa Australia Byron Adu, 25, alishika nafasi ya pili akifuatiwa na Rick Dean Twombley, 33, mcheza dansi toka Hong Kong aliyeshika nafasi ya tatu huku Mhispania Sergio Lara, 26, akishika nafasi ya tano na Mulokozi Rugaimkamu Ngaiza “Mhaya” kutoka Bongo kuchukua nafasi ya Sita. Mashindano ya kwanza ya kumtafuta mrembo wa dunia wa mashoga yalifanyika mwaka jana nchini Canada ambapo mwanaume toka Kagera “TZ” alitwaa taji hilo.