Mtoto mmoja mdogo alikuwa akiongea na baba yake kuhusu suala la kuoa na mazungumzo kati ya wawili hao yalikuwa kama ifuatavyo:
Mtoto: Baba mimi nataka kuoa!
Baba: Mh! Unataka kumuoa nani?
Mtoto: Nataka kumuoa bibi
Baba: We mtoto, yaani unataka kumuoa mama yangu, haiwezekani na hata mila na desturi zetu haziruhusu
Mtoto: Kama haiwezekani mimi kumuoa mama yako mbona wewe umemuoa mama yangu?
Baba akabaki hana jibu...
ZE NO IS NOT RICHABO
Kuna jamaa mmoja hivi juzi aliwaacha watu hoi maeneo ya Posta jijini Dar baada ya kujaribu kupiga simu ya mkononi kumpigia swahiba wake lakini simu ya jamaa yake ilikuwa haipatikani ila simu ilipomjibu jamaa huyo kuwa "Namba ya simu uliyopiga kwa sasa haipatikani tafadhali jaribu tena baadaye". Ndipo jamaa alipoonekana akijibu simu hiyo kwa "We mpumbavu nini unanifanya mimi sina akili sio kama hii simu haipatikani mbona wewe umepokea sasa hebu mpe simu mwenye simu niongee nae bwege wewe.
Watu waliokuwa karibu na jamaa huyo walivunjika mbavu kwa ajili ya kucheka...[center]