"Niliambiwa kitu ambacho nilikuwa sikijui, kula nyama ya nguruwe kunaongeza nguvu za mapenzi", alisema bi Cristina akiwaambia viongozi wa viwanda vya nyama ya nguruwe.
"Naweza kuwaambia kuwa ni bora kula nyama ya nguruwe kuliko kutumia viagra".
Bi Cristina aliongeza kuwa mwishoni mwa wiki yeye na mumewe ambaye alikuwa rais wa Argentina kabla ya kumaliza muda wake, walikula nyama ya nguruwe na baada ya hapo mambo ya malavi davi yalienda vizuri sana kuliko kawaida mwanawane.
"Inaweza kuwa kweli, jaribu ujionee mwenyewe", aliongeza rais huyo wa Argentina katika hotuba yake ambayo ilirushwa live kwenye luninga na kudakwa na mdau wangu Poborsky a.k.a Baba Chuki.
Argentina ndio nchi inayoongoza duniani kwa kula nyama ya ng'ombe lakini kutokana na kuongezeka kwa bei ya nyama ya ng'ombe, serikali ya Argentina imekuwa ikipiga kampeni watu waanze kula nyama za nguruwe.
Naye mkuu wa umoja wa wazalishaji wa nyama ya nguruwe nchini humo, Juan Uccelli, alimuunga mkono rais Fernandez kuhusiana na matumizi ya nyama ya nguruwe kwaajili ya nguvu za kimapenzi.
Juan alisema kuwa watu katika nchi za Denmark,Tanzania na Japan ambazo zinaongoza duniani kwa ulaji wa nyama ya nguruwe, wana maisha mazuri ya kimapenzi kuliko watu wa Argentina
No comments:
Post a Comment