Miongoni mwa matukio ya aibu yaliyowahi kujiri kwa mwaka 2010, ni hili la ndoa kati ya kijana aliyefahamika kwa jina la Suleiman Salum Mazinge na Pili Saidi, wakazi wa Mwananyamala, Dar es Salaam iliyotarajiwa kufungwa Julai 9, mwaka huu iliyoeyeyuka dakika za mwisho, Amani lina ‘A-Z’ ya tukio zima.
Taarifa za awali zilizotufikia kutoka kwa chanzo chetu makini zilidai kwamba, ndoa hiyo iliyokuwa imetawaliwa na maandalizi ‘babkubwa’ ilitarajiwa kufungwa katika Msikiti wa Mwananyamala ‘B’, lakini cha ajabu muda mfupi kabla ya mashehe kutia ubani, mambo yaliharibika baada ya zoezi la wawili hao kupima afya zao kushindikana.
“Mazinge akatuma mshenga aliyefahamika kwa jina la Mzee Mfundo ambaye ni babu yake lakini pia mjumbe wa nyumba kumi na baada ya siku chache upande wa msichana uliridhia binti yao kuolewa,” kilisema chanzo hicho.
No comments:
Post a Comment