Tuesday, July 13, 2010

Mlevi Ampanda Mamba Mgongoni.

Mwanaume mmoja wa nchini Marekani, aliyekuwa amelewa chakari amelazwa hospitali baada ya kujeruhiwa na mamba alipoamua kumfanya mamba kama farasi kwa kumdandia mgongoni. Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 36 alifukuzwa baa baada ya kuonekana pombe zimemzidia ndipo alipoamua kwenda kwenye bustani ya wanyama ya mjini Wichita, Kansas nchini Marekani.

Mwanaume huyo aliipanda fensi na kuingia kwenye bustani hiyo kabla ya kujisogeza kwenye sehemu ambayo wametengewa mamba.

Katika tukio hilo lililotokea kwenye majira ya saa nne usiku, mwanaume huyo alimsogelea mamba mwenye urefu wa mita 2.8 na kujaribu kumnyeshwa bia kabla ya kuamua kurukia kwenye mgongo wa mamba huyo aliyepewa jina la El-Dorado.

"Alitoka kwenye eneo hilo na kwenda kwenye eneo jingine ambalo lilikuwa na mamba mwenye urefu wa mita 5", alisema msemaji wa polisi na kuongeza "Aliona ni wazo zuri kukaa juu ya mamba huyo aendeshwe kama farasi".

"Mamba alijipindua na kuung'ata mguu wake", alisema msemaji huyo wa polisi.

Alifanikiwa kuchoropoka akiwa amejeruhiwa vibaya sana, aliwahishwa hospitali kwa matibabu zaidi.

"Ana bahati sana kuwa hai hadi leo, mtu mwenye akili timamu hawezi kukaa juu ya mamba mwenye urefu wa mita 5", alisema afisa mwingine wa polisi.

Taarifa zinasema kuwa mmiliki wa bustani hiyo hana mpango wa kumfungulia mashtaka mwanaume huyo.

No comments:

Mambo ya kawaida jamani...

Kama unaona kuwa kuna kitu kinakufurahisha humu kwenye blog yangu basi hakuna noma kama ukiniangushia sifa mwanangu mwenyewe.....
Washkaji Mungu akipenda tutaonana basi.........ila kumbuka kuwa Mungu ni mmoja na siku zote anafanya maajabu kwahiyo si mbaya kama tukimshuru kwa kila nia.....
Mungu awabariki watu wote wa Dunia hii.Amen!

9 Things I Hate About Everyone

1. People who point at their wrist while asking for the time.... I know where my watch is pal, where the hell is yours? Do I point at my crotch when I ask where the toilet is?



2
 People who are willing to get off their ass to search the entire room for the T.V.. remote because they refuse to walk to the T.V. and change the channel manually. 

3
 When people say 'Oh you just want to have your cake and eat it too'. Damn right! What good is cake if you can't eat it? 

4
 When people say 'it's always the last place you look'. Of course it is. Why the hell would you keep looking after you've found it? Do people do this? Who and where are they?   cause I amGonna Kick their asses! 

5
 When people say while watching a film 'did you see that?'. No Loser, I paid $12 to come to the cinema and stare at the damn floor. 

6
 People who ask 'Can I ask you a question?'.... Didn't really give me a choice there, did ya sunshine? 


7.
 When something is 'new and improved!'. Which is it? If it's new, then there has never been anything before it. If it's an improvement, then there must have been something before it, couldn't be new.

8
 When people say 'life is short'. What the hell?? Life is the longest damn thing anyone ever does!! What can you do that's longer?




9
 When you are waiting for the bus and someone asks 'Has the bus come yet?'. If the bus came would I be standing here, dumbass? 

 

If you are having a bad day, remember it could be worse...

If you are having a bad day,  remember it could be worse...