
Taarifa hiyo iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, jijini Dar es Salaam na kunifikia mimi kwenye Blog yangu leo asubuhi.
Taarifa hiyo ilisema kikao hicho kitakachoanza kesho na kumalizika Januari 30, mwaka huu, kinahudhuriwa na viongozi wakuu wa nchi, wachumi, viongozi wa mashirika mbalimbali, wanataaluma, viongozi wa dini na wanaharakati mbalimbali duniani.
Mara baada ya kikao cha Davos, Rais Kikwete ataelekea Addis Ababa, Ethiopia kuhudhuria kikao cha kila mwaka cha Wakuu wa Nchi za Afrika, kitakachoanza Januari 31 hadi Februari 2, mwaka huu na kurejea nchini.
No comments:
Post a Comment