Haya yanafuatia hali ya kiuchumi katika klabu hiyo ambayo wengi sasa wanadhani kuwa wamiliki wa klabu hiyo Tom Hicks na George Gillett watashawishika kumuuza mshambuliaji huyo ikiwa kama ofa kubwa itakuja.
Hata hivyo kwa upande wake Benitez anadai kuwa kwa mamlaka yake mshambuliaji huyo hatouzwa kwa gharama yoyote, na kama ikitokea hivyo, basi yupo tayari kujiuzulu.
Katika msimu uliopita Liverpool ilitumia kiasi cha paundi za Uingereza milioni £20, kumleta Anfield, Alberto Aquilani jambo ambalo linaonekana kuwa ni matumizi makubwa, na Benitez anasema kwa jinsi hali ilivyo kiuchumi, hawezi kushindana na timu kama Manchester United na Chelsea katika kipindi cha usajili.
Akitete usajili wake, Benitez anasema "pale walipolazimika kutumia fedha, basi usajili wao umekuwa na mafanikio na akatoa mfano wa usajili wa Torres, Javier Mascherano, Pepe Reina na Xabi Alonso.
Kwa usajili wa Robbie Keane, mhispania anasema huyo ni mshambuliaji mzuri,ila walilazimika kumuuza kutokana na kushindwa kuwaridhisha na kiwango walichokitarajia.
Ryan Babel, kwa huyu anasema alisajiliwa kwa mipango ya baadae na sasa bado wanaendelea kumshinikiza akaze msuli ili apate nafasi katika kikosi cha kwanza.
Kwa sasa Liverpool bado inasuasua katika ligi kuu ya England ikiwa imesimama katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi, baada ya kupoteza michezo mitano katika ligi hiyo msimu huu.
Najua wapenzi wana wasiwasi..anasema Benitez lakini amewataka wawe na subra kwani timu itakuwa sawa na matokeo yatawaridhisha.
No comments:
Post a Comment